Home Reflections Musings & Rants

Category: Musings & Rants

Post
Je, Fasihi ya Kiswahili Inakufa?

Je, Fasihi ya Kiswahili Inakufa?

Kauli kali na tata aliyotoa mshairi mheshimiwa Taban Lo Liyong miaka ya sitini kuwa Afrika Mashariki ni ‘jangwa kifasihi’ imetawala mijadala nyingi kuhusu uwezo wa Mwafrika kubuni sanaa. Mjadala ufuatao wa wapenzi wa fasihi ya Kiswahili ulianzishwa na malalamiko ya Papa Were kuwa ukiritimba umekithiri fasihi ya Kiswahili. Ni mjadala unaofaa kuendelezwa na zaidi ya...